Ziwa Elmenteita, pia Elementaita, ni ziwa la soda/magadi, katika eneo la mashariki la Bonde la Ufa, kilimita 120 kaskazini magharibi mwa Nairobi, Kenya.
Elmenteita ni jina la kiMasaai kutoka neno muteita, maana yake "mahali penye vumbi", ikimaanisha vumbi na ukavu wa eneo hilo, hasa kati ya Januari na Machi. Mji wa Gilgil uko karibu na ziwa. Ukianzia kusini-kuelekea-kaskazini mwa maziwa ya Bonde la Ufa, Elmenteita iko kati ya Ziwa Naivasha na Ziwa Nakuru. Barabara Kuu yaNairobi - Nakuru hupitia karibu na bonde hivi kwamba watumia magari huvutiwa na mandhari ya ziwa hili.
Kusini mwa ziwa moto chemchem wa "Kekopey" huchipua, ambapo Grahamii Tilapia hukua. Maarufu Sana kwa kuoga, Masai hudai kwamba wanaweza kutibiwa ukimwi wakiwa mahala hapa. Reedbeds ni eneo la uvuvi kwa ndege aina ya Night Heron na Mwari.
Ziwa Elmenteita liliona makazi yake ya kwanza ya mkoloni wakati Bwana Delamere (1879-1931) aliweka Soysambu, a 48,000-acre (190 km2) ranch, upande wa magharibi wa ziwa. Delamere alimpa shemejiye kipande cha ardhi karibu na ziwa , hishima Galbraith Lowry Egerton Cole (1881-1929), sehemu ambapo yeye alizikwa, inayolindwa leo kama Ziwa Elementaita.
Soysambu bado inadhibitiwa na jamaa yake, akiwemo PG Thomas Cholmondeley. Eneo hili ni makao kwa zaidi ya wanyama 12,000 wa pori.
Ziwa Elmenteita imekuwa mandhari ya Ramsar tangu mwaka 2005.
Ndege wa aina 400 tofauti wamewekwa katika kumbukumbu katika Ziwa Nakuru / Ziwa Elmenteita . Elmenteita huvutia flamingo, ambao hula wadudu na mwani. Tilapia walihamishwa kutoka Ziwa Magadi mwaka 1962 na tangu wakati huo idadi ya Flamingo imepungua mno. Tilapia huvutia ndege wengine ambao hula samaki hawa na hata pia mayai ya Flamingo na vifaranga vyake. Zaidi ya ndege milioni hivi hamehama Ziwa Elmenteita na kukimbilia katika Ziwa Natron nchini Tanzania.
Ufuo wa Ziwa una Zebra, gazelle, Eland na familia ya ngiri.
Ziwa hili kawaida lina kimo cha chini (<1 m kirefu).
Hivi karibuni ngazi ya ziwa na idadi ya flamingo inapungua kutokana na ongezeko ya shughuli za binadamu