Saba ni kisiwa cha bahari ya Karibi (Amerika ya Kati). Kwa kiasi kikubwa kinaundwa na volkeno inayoweza bado kulipuka. Urefu wake ni mita 887.
Ni sehemu ya pekee ya Uholanzi.
Eneo lake, pamoja na kisiwa kidogo cha jirani (Green Islet), ni kilometa mraba 13 tu.
Wakazi wa kudumu ni 1,991. Wengi wao ni machotara, ni Wakristo wa Kanisa Katoliki na huongea hasa Kiingereza, ingawa Kiholanzi ndicho lugha rasmi.
Makao makuu ni The Bottom.