thumb|300px|Chemchemi za moto za Pamukkale
Pamukkale (Kituruki: Boma la pamba) ni kijiji katika Uturuki wa kusini-magharibi pamoja na maajabu asilia inayohesabiwa kwenye mahali pa urithi wa dunia.
Maajabu ya Pamukkale ni maporomoko ya maji ya moto yenye kiwango kikubwa cha chumvi ya chokaa. Chokaa hiki kiliganda kwa karne nyingi ikajenga ngazi za rangi nyeupe zinazovuta watalii wengi.
Maghofu ya mji wa kale wa Hierapoli ni karibu na kijiji cha leo.