Oaxaca (jina rasmi: Oaxaca de Juárez) ni mji mkuu na mji mkubwa katika jimbo la Oaxaca. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mnamo mwaka wa 2005, mji una wakazi wapatao 258,008 wanaoishi katika mji huu. Eneo lake ni 258 km².
Mji ulianishwa na Wahispania mwaka 1522.