Kanisa Kuu la Azania Front

Kanisa Kuu la Azania Front (kwa Kiingereza Azania Front Cathedral) ni kanisa kuu la Walutheri lililopo jijini Dar es Salaam katika wilaya ya Ilala na ni moja kati ya vivutio vya jiji hilo la Tanzania.

Kanisa hili lipo katika barabara ya Kivukoni karibu na Waterfront, mkabala na hoteli ya New Africa na feri kuelekea mji wa Kigamboni.

Jina la Azania Front linatokana na jina la awali la barabara ya Kivukoni Front iliyopo baina ya kanisa na ufukwe wa bahari.

Historia

Kanisa hili lilijengwa kwa gharama za mark 180,000 kuanzia mwaka 1899 baada ya kufika kwa mchungaji wa kwanza aliyetumwa kwa ajili ya Wajerumani wa Dar es Salaam. Ilifunguliwa rasmi tarehe 21 Mei 1902 ikawa kanisa la Walutheri Wajerumani katika mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.

Baada ya kufukuzwa kwa Wajerumani wa mwisho mwaka 1920 jengo lilitumiwa na ushirika wa Kianglikana. Tangu mwaka 1925 Wajerumani waliruhusiwa kurudi Tanganyika iliyokuwa sasa chini ya Uingereza na kanisa likarudi mikononi mwa kanisa la Kilutheri likatumiwa kwa ibada za Wajerumani na pia za ushirika wa Kiafrika.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Wajerumani walifukuzwa tena na tangu siku zile hilo ni kanisa kuu la Waluteri Waafrika. Hadi sasa linasimama kama alama katika mji na hivyo limeorodheshwa kati ya kumbukumbu za taifa.

Altari ya kanisa lina maandishi kwa lugha ya Kijerumani: "Den Frieden lasse ich euch, meinen Frieden gebe ich euch" ("Amani nawaachieni; amani yangu nawapa", Yoh 14:27)

Upekee wa ujenzi wa kanisa hili unashuhudia utajiri wa ujenzi katika mji.

Marejeo

  • H. Tscheuschner, Geschichte der Deutschen Gemeinde in Dar es Salaam von 1886 bis 1969, Dar es Salaam 1970 (Historia ya Ushirika wa Kijerumani wa Dar es Salaam 1886 hadi 1969, mswada)

Viungo vya nje

Imeorodheshwa katika kategoria zifuatazo:
Tuma maoni
Vidokezo na Vidokezo
Myoma Kapya
14 May 2012
Knowing Christ is a life changing experience
Pakia maoni zaidi
foursquare.com
6.5/10
5,645 watu wamekuwa hapa
Ramani
0.1km from Kivukoni Rd, Dar es Salaam, Tanzania Pata maelekezo

Azania Front Lutheran Church kwenye Foursquare

Kanisa Kuu la Azania Front kwenye Facebook

Best Western CBD Hotel

kuanzia $94

New Yuetan Hotel

kuanzia $30

Iris Hotel

kuanzia $32

Sleep Inn Hotel Kariakoo

kuanzia $32

Peacock City Centre

kuanzia $77

ABC Travellers Hotel

kuanzia $30

Vitunguu vilivyopendekezwa karibu

Ona yote Ona yote
Ongeza kwenye orodha ya matamanio
Nimekuwa hapa
Walitembelewa
Sanamu ya Askari

Sanamu ya Askari au Askari Monument ni sanamu iliyopo penye kitovu cha

Ongeza kwenye orodha ya matamanio
Nimekuwa hapa
Walitembelewa
Kanisa la Mtakatifu Joseph

Kanisa la Mtakatifu Joseph (kwa Kiingereza: St Joseph Cathedral

Ongeza kwenye orodha ya matamanio
Nimekuwa hapa
Walitembelewa
Benjamin William Mkapa Pension Tower

Mafuta House is one of the tallest buildings in Dar es Salaam,

Ongeza kwenye orodha ya matamanio
Nimekuwa hapa
Walitembelewa
Daraja la Julius Nyerere

Daraja la Kigamboni ni daraja ambalo linavuka mkondo wa Kurasini

Ongeza kwenye orodha ya matamanio
Nimekuwa hapa
Walitembelewa
Makatumbe Range Rear Lighthouse

The Makatumbe Range Rear Lighthouse (also known as Dar es Salaam Bay

Ongeza kwenye orodha ya matamanio
Nimekuwa hapa
Walitembelewa
Uhuru Monument

The Uhuru Monument (also known as Uhuru Torch Monument) is a landmark

Ongeza kwenye orodha ya matamanio
Nimekuwa hapa
Walitembelewa
Hifadhi ya bahari ya Dar es Salaam

Hifadhi ya bahari ya Dar es Salaam inajumlisha maeneo kadhaa kwenye

Ongeza kwenye orodha ya matamanio
Nimekuwa hapa
Walitembelewa
Kaole

Kaole ni mji mdogo na wa kihistoria unaopatikana katika ufukwe wa

Vivutio sawa vya watalii

Ona yote Ona yote
Ongeza kwenye orodha ya matamanio
Nimekuwa hapa
Walitembelewa
St. Lorenz, Nuremberg

St. Lorenz (St. Lawrence) is a medieval church of the former free

Ongeza kwenye orodha ya matamanio
Nimekuwa hapa
Walitembelewa
Temppeliaukio Church

Temppeliaukio Church (Temppeliaukion kirkko in Finnish, Tempelplatsens

Ongeza kwenye orodha ya matamanio
Nimekuwa hapa
Walitembelewa
Evangelicko-luteránská katedrála sv. Petra a Pavla v Moskvě

Petrus- en Pauluskatedraal

Ongeza kwenye orodha ya matamanio
Nimekuwa hapa
Walitembelewa
St. Thomas Church, Leipzig

The Thomaskirche (St. Thomas Church) is a Lutheran church in Leipzig,

Ongeza kwenye orodha ya matamanio
Nimekuwa hapa
Walitembelewa
Sankt-Annen-Kirche (Sankt Petersburg)

Це́рковь Свято́й А́нны (Deutsch. Annenkirche - Анненкирхе) — лютер

Tazama maeneo yote yanayofanana