Mbuga ya Taifa ya Mlima Kenya , iliyoanzisha mwaka wa 1949, hulinda kanda inayozunguka Mlima Kenya. Awali ilikuwa ni hifadhi ya misitu kabla ya kutangazwa kama mbuga ya kitaifa. Hivi sasa ni mbuga ya taifa ndani ya hifadhi ya misitu ambayo imeizunguka.Mnamo Aprili mwaka wa 1978 eneo hilo lilifanywa hifadhi ya Biosphere ya UNESCO. Mbuga ya taifa na hifadhi ya misitu ziliunganishwa zikawa katika orodha ya Urithi wa Dunia wa UNESCO mwaka wa 1997.