Efeso (kwa Kigiriki Έφεσος) uliwahi kuwa moja kati ya majiji ya dunia.
Lilianzishwa na Wayunani huko Lidia mto Kaistro unapoishia katika Bahari ya Kati, kwenye pwani ya Uturuki wa leo.
Lilikuwa kituo kikubwa cha biashara na magofu yake ni kati ya mahali muhimu pa akiolojia.
Mtume Paulo aliishi huko miaka mitatu akawaandikia Wakristo wake barua muhimu.
Baadaye alihamia huko Mtume Yohane ambaye pia katika Kitabu cha Ufunuo aliandika barua kwa malaika wa Kanisa hilo pamoja na 6 nyingine kwa malaika wa Makanisa ya kandokando.