Ukuta mkubwa wa China ni kati ya majengo makubwa kabisa yaliyojengwa duniani. Una urefu wa kilomita 6,400 kuanzia bahari ya China hadi jangwa la Taklamakan ukifuata mpaka kati ya China na Mongolia ya kihistoria.
Ukuta ulijengwa na nasaba mbalimbali za watawala wa China tangu mwaka 200 KK. Shabaha yake ilikuwa ulinzi wa milki dhidi ya mataifa na makabila wa kaskazini walioendelea kushambulia China. Watu wa kaskazini walikuwa wahamiaji waliotumia farasai na ngamia hivyo haukuwa rahisi kujua ni wapi watakaojaribu kuingia.
Ukuta jinsi ilivyo ni ukuta wa nasaba ya Ming uliojengwa kuanzia mnamo mwaka 1500. Manmo mwaka 1700 ukuta haukutunzwa tena kwa sababu katika karne ya 17 sehemu kubwa za Mongolia nje ya ukuta ziliunganishwa na China.
Ukuta huwa na upana kati ya mita 4 hadi 8 m na kimo cha mita 6 hadi 9. Kila baada ya mita mamia minara ilijengwa ukutani. Minnara hii ilikuwa vituo vya kulala kwa walinzi pia ngome zao waati wa kushambuliwa na vitua vya mawasiliano kati ka mnara na mnara. Kwa jumla ukuta ulikuwa na minara 25,000.